Na Editha Karlo - Malunde1 blog Kigoma.

ASKARI wawili wa Jeshi la wananchi(JWTZ) kikosi cha 24KJ Mkoani Kigoma,wamefariki dunia na wengine zaidi ya kumi kujeruhiwa katika ajali iliyotokea leo kwenye hifadhi ya Katavi.

Askari hao wamepata ajali baada ya gari la jeshi lililokuwa limebeba silaha kupinduka wakati wakielekea kwenye oparesheni Mkoani Katavi.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma maweni Lameck Mdengo amethibitisha kupokea majeruhi hao pamoja na maiti mbili.

"Ili kuwa majira ya saa 8 tulipokea majeruhi 20 na wawili wakiwa wamefariki dunia ambao tumewapatia huduma ya kwanza,wapo waovunjika mikono na miguu pia lakini tunafanya utaratibu kuwapa rufaa ya kwenda Muhimbili au Bugando"alisema

Aliwataja waliofariki ni Bakari juma Mohamed,Rashid Abed Mwimbe
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: