Masanduku maalumu kwa ajili ya uwekaji wa kura yakiwa yameandalia kwa ajili ya wajumbe wa mkutano mkuu wa Jimbo la Hai kumchagua kada atakaye peperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu unatarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu
Msimamaizi wa Uchaguzi katika jimbo la Hai Kataba Sukuru akizungumza wakati wa zoezi la utangazaji wa matokeo katika uchaguzi huo .
Mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya na Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ni miongoni mwa wajumbe walioshiriki katika kufanya uamuzi wa kumpata kada atakaye peperusha bendera ya Chama hicho.
Baadhi ya Wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo la Hai wakiwa katika maandalizi ya zoezi la upigaji kura.
Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya akiwa amebeba karatasi ya kura tayari kwenda kumchagua kada atakaye peperusha bendera katia jimbo la Hai.
Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya akipiga kura yake.
Lengai Ole Sabaya akitumbukiza kura yake katika sanduku la kura.
Wajumbe wakiwa katika foleni ya kwenda kupiga kura.
Baadhi ya wagombea wakingojea maamuzi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo la Hai wa nani atawavusha katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu .
Huyu ni Saashisha Mafuwe Mshindi wa kura za maoni katika jimbo la Hai .
Mgombea wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Hai ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Saashisha Mafuwe akiwa amebebwa juu mara baada ya kutangazwa mshindi wa kura za maoni ambapo wajumbe walimpigia kura 124

Na Dixon Busagaga, Hai

Mgombea ubunge katika jimbo la Hai katika kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) na kada wa chama hicho Saashisha Mafuwe ameibuka mshindi baada ya kupigiwa kura 124 na wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo hilo.

Hatua hiyo ni hitimisho la chaguzi za ndani ya  Chama cha Mapinduzi  za kura za maoni katika ngazi ya majimbo ambapo majimbo manne kati ya tisa ya mkoa wa Kilimanjaro yalikuwa yamesalia baada ya zoezi hilo kuanza siku Jumatatu.

Majimbo yaliyokuwa yamesalia katika uchaguzi uliofanyika Jumatatu ni pamoja na jimbo la Moshi vijijini,Jimbo la Hai na Jimbo la Same Magharibi .

Katika uchaguzi wa jimbo la Hai Mafue ambaye ni mtumishi kati tume ya madini amewashinda aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo la Hai  Fuya Kimbita aliyepata kura 85 akifuatiwa na Abubakar Msangi aliyepata kura 48  kati ya wagombea 42 waliojitokeza kuwania nafasi hiyo.

Katika Jimbo la Moshi vijijini wagombea walikuwa ni 47 waliorejesha fomu huku wagombea 46 wakijitokeza kuwania nafasi hiyo ,mpambano mkali ukikua baina ya Prof Patrick Ndakidemi,Deogratius Mushi na Moris Makoye .

Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo la Moshi mjini Asia Halamga akamtangaza Profesa Patrick Ndakidemi kuwa mshindi baada ya kuibuka kura 262 akiwashinda Deogratius Mushi aliyepata kura 46 akifuatiwa na Moris Makoi .

Katika jimbo la Same Magharibi ,Mbunge anayemaliza muda wake Dkt Mathayo David ametetea nafasi yake baada ya kupata kura 389 dhidi ya kura 300 za mshindani wake aliyemfuatia Angela Kairuki huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na Marry Mgonja aliyepata kura 18.

Hatua ya awali ya uchaguzi katika majimbo ya mkoa wa Kilimanjaro umemalizika huku majina ya walioshika nafasi za juu yakitaraji kupelekwa katika vikao  vya Chama cha Mapinduzi kwa ajili ya mapendekezo na maamuzi .

Chama cha Mapinduzi kwa sasa kinajielekeza katika Chaguzi za kura za maoni kwa Wabunge watakaotokana na viti maalumu zoezi linalotarajia kufanyika siku ya Alhamisi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: