Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt Philemon Sengati akizungumza jana na waandishi wa habari wakati akitoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa.

NA TIGANYA VINCENT.

WAKAZI Mkoa wa Tabora wamepokea kwa masikitiko kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa na kusema kuwa Taifa limepoteza kiongozi imara.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati wakati mkutano na waandishi wa habari Ofisini alipokuwa akitoa salamu za rambirambi za Mkoa huo.

Alisema wakazi wa Mkoa wa Tabora watambuka Mhe. Mkapa kwa kuiwezesha Nchi kuondoka katika hali mbaya ya Auchumi na kujenga misingi imara ya uchumi na maendeleo ya nchi.

Dkt. Sengati alisema katika enzi za utumishi wake kama Kiongozi wa Nchi aliweza kubana matumizi na kujenga nidhamu ya matumizi ya fedha za serikali na kupunguza rushwa.

Aliongeza kuwa katika kipindi chake aliweza kuanzisha harakati za kufufua uchumi kwa kuanzisha Taasisi muhimu kama vile Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) , Taasisi za Maadili na nyingine ambazo zilisaidia kuongeza makusanyo ya Serikali na kusimamia nidhamu kwa watumishi wa umma.

Dkt Sengati watanzania wanatakiwa kuiga kwa Mhe. Mkapa kwa kupenda kumucha Mungu na kuishi kwa kuzingatia maagizo yake ili kuendelea kufanya mema na kuachana na maovu.

Alisema hatua hiyo itasaidia kuipenda Tanzania kama alivyokuwa akifanya Mkapa wakati wa uhai wake na kupenda kuipeleka Nchi mbele.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: