Na Charles James, Michuzi TV

ULIBADILISHA Maisha yetu, ulitujali maskini, ulijenga vituo vya afya, ulipambana na mafisadi, ukatoa elimu bure kwa watoto wetu. Nenda Dk John Magufuli kiongozi na mtumishi wetu.

Hizo ni kauli na vilio vya wananchi wa Mkoa wa Mwanza na mikoa jirani ya Kanda ya Ziwa ambao wamejitokeza kwa wingi kwenye barabara ya mitaa ya Mwanza kumuaga aliyekua Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli.

Shughuli za kuuaga mwili wa Hayati Dk Magufuli zimefanyika katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo wananchi waliopata nafasi ya kuingia uwanjani hapo walipata fursa ya kumuaga kwa gari lililobeba mwili wake kuzunguka mara tano ndani ya uwanja huo.

Baada ya kumaliza kuzunguka ndani ya uwanja mwili wa Dk Magufuli unapitishwa kwenye mitaa ya jiji la Mwanza ikiwemo mitaa ya Benki Kuu, Nyegezi, Mabatini, Igogo na sehemu nyinginezo.

Baada ya kumaliza kuagwa kwenye Jiji la Mwanza msafara wenye mwili wa Dk Magufuli utaelekea nyumbani kwake Chato lakini utasimama eneo la Busisi ambapo ni nyumbani kwa wakwe zake yaani nyumbani kwa wazazi wa Mama Janeth Magufuli kwa ajili pia ya kuagwa.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: