Amir Mkuu wa taasisi hiyi akizungumza wakati wa tukio hilo la uchangiaji damu

Na Mwandishi Wetu

WANAFUNZI wa Shule ya Ilala Islamic ya jijini Dar es Salaam wamechangia damu kwenye Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Amana jijini ikiwa ni hatua ya kuunga mkono jitihada za kuchangia damu ili isaidie wenye uhitaji.

Tukio hilo la uchangiaji damu katika hospitali hiyo lilikuwa limeandaliwa na Taasisi ya Jamii yetu Akhraqual Islamic( JAI) iliyoongozwa na Amir Mkuu wa taasisi hiyo.

Akizungumza kwenye uchangiaji damu huo Amir Mkuu huyo katika taasisi hiyo Sheikh Yahya Ally amesema ni vema kila mtu kwa nafasi yake kujitokeza kuchangia kutokana na uitaji kuwa mkubwa wa damu.

"Hospitali kadhaa bado kuna mahitaji makubwa ya damu na kwa kutambua hilo sisi kama taasisi tumeamua kujitolea kuchangia damu katika kuisadia jamii na kwao ikiwa ni sehemu ya ibada," amesema Shekhe Yahya.
Kwa upande wake Mganga Mkuu amesifia uchangiaji wa damu lililofanywa na taasisi hiyo ya JAI lililofanyika katika hospitalini hapo na engo lilikuwa ni kupata watu takribani 300 ambapo kwa siku mahitaji ya hospitali hiyo ni chupa 30 hadi 50.

"Kila siku tumekuwa tukisisitiza kuchangia damu kutokana na uhitaji mkubwa wa damu uliopo ni vyema watanzania kuendelea kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wahitaji ikiwemo watoto, wajawazito pamoja na wanaokuja hapa kwa ajali za barabarani ," amesema Dk.Malima.

Kwa upande wake mwanafunzi Amina Omari anayesoma kidato cha tano shule ya sekondari Ilala Islamic wasichana mchepuao wa sayansi amesema wameamua kuchangia damu kwani mahitaji ni makubwa kwa wagonjwa ya kina mama na wajawazito .

" Tunaiunga mkono Serikali kwani imekuwa ikisisitiza jamii kuchangia damu chini ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama Tanzania, chini ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto,"amesema Amina.

Aidha kwa upande wake Ofisa Muhamasishaji Jamii Damu Salama kanda ya Mashariki Mariamu Juma amesema wapo wanaopoteza maisha kwa kupoteza damu nyingi sana na wengine ni waanga wa ajali mbali mbali.

"Damu ni tiba na kazi yetu ni kuamasidha jamii kuokoa wagonjwa ndiyo maana ni tiba kwa waanga mbali mbali,"amesema Mariam.

Wakati mwanafunzi Nasibu Mussa anayesoma mchepuo wa sayansi kitato cha tano katika shule ya sekondari Ilala Islamic wavulana amesema wamefika kuchangia damu kwa ni ni jambo ambaro wananusuru maisha ya watu wanaoitaji damu wakiwa hospitalini kwa matatizo mbali mbali.

Mmoja wa wazazi walioshiriki uchangiaji huo wa damu Fatuma Hamad amesema wamefika kuwaunga mkono mwanafunzi wao kwani asilimia kubwa wameonekana kufika Hospitalini hapo kwa wingi.Katika kuchangia damu huko pia kulihusisha makundi mengine kwenye jamii.

Kuhusu shule hiyo,imeelezwa waka 2020/21 imepata matokeo bora ambapo wanafunzi 36 walipata daraja la kwanza na sita kupata daraja la pili hata hivyo hapakuwa na daraja la tatu, nne na Ziro kitu kilichoifanya shule hiyo kushika nafasi ya 9 kimkoa na 80 kitaifa katika zaidi ya Shule 5000.

juhudi zao ndizo ndizo zinazosababisha shule hiyo kujipatia tunzo kutoka kwenye taasisi mbalimbali ambapo mwaka 2016 walipata kupata tunzo katika mashindano ya kawaida ya Ramadhani Quiz pamoja na yale ya Wizara ya elimu, kwa shule binafsi shule hiyo ilishika nafasi ya nne pia ikaja kushika nafasi ya tatu, ya kwanza sambamba na kukamata nafasi ya pili ndani ya miaka saba mfululizo.

Aidha shule ya bweni na kutwa inayosimamiwa katika misingi bora ya dini ya Kiislamu kwa kuwafundisha vijana namna ya kushiriki vema katika shughuli mbalimbali za kitaifa na zile za kidini. Wakati malengo ya walimu wamejikita kuwaandaa vijana kuwa na maadili mema ndani ya jamii hatua inayopelekea kuweza kupata matokeo mazuri na bora.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: