Mashabiki wa Ligi Kuu ya England nchini Tanzania wanajiandaa kushuhudia tukio la kipekee baada ya Kombe la Ligi hiyo kutua rasmi nchini kwa mara ya kwanza kupitia Guinness, Mdhamini Mkuu wa Bia wa Ligi Kuu ya England.

Kombe hilo litawasili nchini Ijumaa, Oktoba 9, 2026, kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) majira ya saa tatu asubuhi, kabla ya kuzungushwa katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam ili kuwapa mashabiki fursa ya kuliona kwa karibu.

Hivyo, kwa mashabiki wa EPL ambao wamezoea kuliona Kombe hilo likikabidhiwa baada ya msimu kumalizika kupitia televisheni, safari hii litakuwa mbele yao na katika jiji lao.Baada ya kuzunguka katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, Kombe hilo litahamia The Super Dome, Masaki, ambako kutakuwa na hafla maalum kwa wageni na mashabiki kupata fursa ya kuliona kwa karibu zaidi na kupiga picha nalo.
Akizungumzia ujio wa Kombe hilo, Mkurugenzi wa Ubunifu na Masoko wa Serengeti Breweries Limited (SBL), Henry Esiaba, alisema Guinness inaleta uzoefu wa EPL karibu zaidi na mashabiki wa soka nchini.

“Mashabiki wa Tanzania wana mapenzi makubwa na Ligi Kuu ya England na kila wiki wanafuatilia mechi, wanajadili timu zao na kusherehekea pamoja. Safari hii tunataka kuwapa nafasi ya kuona Kombe lenyewe kwa karibu na kuwa sehemu ya tukio hili. Ni fursa kwa mashabiki kupata uzoefu tofauti na ule wanaoupata wanapotazama mechi kwenye televisheni,” alisema Esiaba.

Burudani ya soka itaendelea Jumamosi, Oktoba 10, ambapo mashabiki watakutana katika Uwanja wa KMC, Mwenge, kwa Guinness Matchday.
Katika tukio hilo, mashabiki watapata fursa ya kushuhudia kwa pamoja mechi za Ligi Kuu ya England kupitia skrini kubwa, ikiwemo mchezo wa Arsenal dhidi ya Leeds pamoja na Manchester United dhidi ya Tottenham Hotspur.

Lakini kwa kuwa soka Tanzania lina ladha yake, siku hiyo pia mashabiki watapata nafasi ya kushuhudia Dabi ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga mubashara kupitia skrini kubwa zitakazowekwa katika eneo la tukio.

Hiyo itakuwa fursa ya mashabiki wa soka kukutana sehemu moja, kufuatilia mechi za Ligi Kuu ya England na wakati huo huo kushuhudia moja ya mechi zinazovuta hisia kubwa zaidi katika soka la Tanzania.Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kampuni wa SBL, Juanita Mramba, alisema ujio wa Kombe hilo unalenga kuwaleta pamoja mashabiki na wadau wa soka kupitia uzoefu unaounganisha soka la kimataifa
“Soka linawajumuisha watu wengi na Tanzania ni moja ya nchi ambazo mashabiki wake wanaishi kwa karibu sana na mchezo huu. Kupitia ujio wa Kombe la EPL, tunataka mashabiki wapate nafasi ya kuliona kwa macho yao, kupiga picha nalo na kushiriki katika matukio yatakayowakutanisha pamoja. Hii ni nafasi ya kusherehekea soka na mashabiki ambao wamekuwa sehemu muhimu ya utamaduni wa mchezo huu,” alisema Juanita.

Mbali na kutazama mechi, mashabiki watakaohudhuria Guinness Matchday watapata pia fursa ya kupiga picha na Kombe la Ligi Kuu ya England, huku wakifurahia burudani na mazingira ya pamoja ya kusherehekea soka.Ujio wa Kombe hilo Tanzania unaifanya Dar es Salaam kuwa sehemu ya ziara maalum ya Kombe la Ligi Kuu ya England katika Afrika Mashariki, huku Guinness ikiendelea kutumia nafasi yake kama Mdhamini Mkuu wa Bia wa Ligi hiyo kuwaleta mashabiki karibu na mchezo wanaoupenda.

Kwa siku mbili, Oktoba 9 na 10, macho ya mashabiki wa soka yataelekezwa Dar es Salaam, kuanzia ujio wa Kombe hilo JNIA, safari yake katika maeneo mbalimbali ya jiji, hafla ya Super Dome Masaki hadi Guinness Matchday katika Uwanja wa KMC, Mwenge.Kwa mashabiki wa EPL na soka kwa ujumla, hii ni nafasi ya kuliona Kombe la Ligi Kuu ya England kwa karibu na kusherehekea soka pamoja na mashabiki wengine.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: