Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania, Harriet Lwakatare, akichangia damu kwa ajili ya kuongeza akiba ya damu katika Benki ya Damu nchini na kusaidia kuokoa maisha ya watu wanaohitaji huduma hiyo. Zoezi hilo ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026, inayoangazia umuhimu wa kuwahudumia wateja huku pia ikichangia ustawi wa jamii.Mchango wa damu una umuhimu mkubwa katika kusaidia wagonjwa wanaohitaji damu wakati wa matibabu na huduma nyingine za dharura.
Tukio hilo limefanyika tarehe 7 Oktoba 2026, jijini Dar es Salaam, likiwa sehemu ya shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Vodacom Tanzania katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 yenye kaulimbiu “Zaidi ya Huduma ni Ukaribu!
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja baada ya tukio la uchangiaji damu wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja. Tukio hilo limefanyika jana jijini Dar es Salaam likiwa sehemu ya shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Vodacom Tanzania katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 yenye kaulimbiu “Zaidi ya Huduma ni Ukaribu”





Toa Maoni Yako:
0 comments: