Benki ya Exim Tanzania imedhamini mbio za kilomita 5 (5KM Fun Run) katika Korosho Marathon 2026, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za kuhamasisha afya bora na ushiriki wa jamii katika michezo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Kanda wa Benki ya Exim Tanzania, Emmanuel Sango, amesema benki hiyo inaendelea kuunga mkono shughuli zinazochangia ustawi wa jamii na kukuza fursa za kiuchumi kwa wananchi.
Ameeleza kuwa sekta ya korosho ni muhimu kwa uchumi wa Mtwara, huku fursa za kuongeza thamani ya zao hilo kupitia usindikaji, biashara na upanuzi wa masoko zikihitaji huduma za kifedha zinazowawezesha wakulima na wafanyabiashara kukuza shughuli zao.
Udhamini wa Korosho Marathon 2026 unaakisi dhamira ya Benki ya Exim Tanzania ya kushirikiana na jamii katika kukuza maendeleo endelevu, kwa kutambua kuwa afya bora ni msingi muhimu wa kuongeza tija na kuchochea ukuaji wa uchumi. Kupitia michezo, benki hiyo inaendelea kuhamasisha mshikamano wa kijamii, kujenga mahusiano na wadau mbalimbali pamoja na kuunga mkono juhudi za maendeleo katika maeneo inakotoa huduma.
Kupitia suluhisho za kifedha zinazokidhi mahitaji mahususi ya wateja, Benki ya Exim Tanzania inaendelea kuwawezesha wakulima, wafanyabiashara na wadau wengine wa sekta ya korosho kupata huduma zinazokidhi mahitaji yao na kuwasaidia kuimarisha shughuli zao katika uzalishaji, usindikaji na biashara ya zao hilo.







Toa Maoni Yako:
0 comments: