
Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania Plc, Philip Besiimire, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Zaidi ya Malipo, Ni Shangwe’, inayolenga kuhamasisha matumizi ya M-Pesa katika kufanya malipo ya bidhaa na huduma mbalimbali msimu huu wa sikukuu. Kupitia kampeni hiyo, wateja wanaokidhi vigezo watapata fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali, zikiwemo magari matano aina ya Jetour T2, pamoja na kurejeshewa hadi asilimia 10 ya fedha kwenye baadhi ya malipo. Kampeni hiyo ilizinduliwa Novemba 27, 2026, jijini Dar es Salaam, katika hafla iliyohudhuriwa na wafanyakazi wa Vodacom, wadau, wasanii na wananchi mbalimbali.

Moja ya magari matano aina ya Jetour T2 yatakayotolewa kama zawadi kuu likitambulishwa rasmi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Vodacom ya ‘Zaidi ya Malipo, Ni Shangwe’, Novemba 27, 2026, jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo inawapa wateja wanaokidhi vigezo fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali kwa kufanya malipo kupitia M-Pesa.

Masta Shangwe akitoa burudani jukwaani wakati wa tamasha la Vodacom Shangwe Festival, lililoambatana na uzinduzi wa kampeni ya ‘Zaidi ya Malipo, Ni Shangwe’, Novemba 27, 2026, jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo inalenga kuhamasisha matumizi ya malipo ya kidijitali kupitia M-Pesa, huku ikiwapa wateja fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali msimu huu wa sikukuu.
Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando pamoja na Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara na Masoko Brigita Shirima, wakizungumza na umati uliohudhuria tamasha la Vodacom Shangwe Festival huku wakiambatana na Kaimu Mkurugenzi wa M-Pesa, Tulisindo Mlupilo, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Zaidi ya Malipo, Ni Shangwe’, Novemba 27, 2026, jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo inalenga kuhamasisha matumizi ya malipo ya kidijitali kupitia M-Pesa, huku ikiwapa wateja wanaokidhi vigezo fursa ya kujishindia magari matano aina ya Jetour T2, vikapu vya zawadi za sikukuu pamoja na kurejeshewa hadi asilimia 10 ya fedha kwa baadhi ya malipo.
Baadhi ya washiriki wa tamasha la Vodacom Shangwe Festival wakifurahia burudani wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Zaidi ya Malipo, Ni Shangwe’, uliofanyika Novemba 27, 2026, jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliwakutanisha wafanyakazi wa Vodacom, wadau, wasanii na wananchi mbalimbali kusherehekea uzinduzi wa kampeni hiyo ya msimu wa sikukuu.
Magari yatakayotolewa kama zawadi kwa wateja yakioneshwa katika eneo la tamasha la Vodacom Shangwe Festival wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Zaidi ya Malipo, Ni Shangwe’, jijini Dar es Salaam. Kupitia kampeni hiyo itakayodumu kwa wiki nane, wateja wanaokidhi vigezo watapata fursa ya kujishindia magari matano aina ya Jetour T2, pamoja na zawadi nyingine mbalimbali.





Toa Maoni Yako:
0 comments: