Neema Temba, Mkurugenzi wa Masuala ya Sheria na Uhusiano TBL (wa pili kulia), na Mkurugenzi wa Maendeleo kutoka Taasisi ya Tanzania Red Cross Society (TRCS), Reginald Mhango (wa pili kushoto), wakizungumza na waandishi wa habari wakati wa kusaini hati ya makubaliano (MoU) ya mpango wa mafunzo ya waendesha pikipiki katika wilaya zote tano za jiji la Dar es salaam yenye lengo la kuepusha ajali za barabarani zinazotokana na uzembe wa waendesha pikipiki. Wengine katika picha ni Afisa Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Tanzania Redcross Society Simon Kadogosa(kulia), na Catherine Mabula, Afisa Mawasiliano TBL.Na

 Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni ya Tanzania Breweries PLC (TBL), kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania (Tanzania Red Cross Society), imewafundisha waendesha pikipiki 1,624 jijini Dar es Salaam kuhusu usalama barabarani na huduma ya kwanza, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupunguza ajali na kuokoa maisha.

Mafunzo hayo yaliyotolewa kupitia ushirikiano ulioanza mwaka 2024 yamevuka lengo la kuwafikia waendesha pikipiki 1,600, na kufikia asilimia 102 ya lengo lililowekwa.

Mafunzo hayo yalifanyika katika wilaya zote tano za Dar es Salaam, yakilenga kuwajengea washiriki uelewa kuhusu uendeshaji salama, sheria na kanuni za barabarani, matumizi sahihi ya helmeti, hatua za kuchukua wakati wa dharura na kufanya maamuzi sahihi wanapotumia barabara.

Akizungumza kuhusu programu hiyo, Mkurugenzi wa Masuala ya Sheria na Uhusiano wa Kampuni wa TBL, Neema Temba, alisema kampuni inaamini kuwa jamii salama ni msingi wa maendeleo na ustawi wa wananchi.

Alisema usalama barabarani unahusisha kulinda maisha ya watu, familia na vyanzo vyao vya kipato, hivyo elimu kwa waendesha pikipiki ni muhimu katika kuzuia ajali na kuhakikisha wanarejea nyumbani salama.

“Usalama barabarani si tu kuzuia ajali; ni kulinda familia, kulinda vyanzo vya kipato na kuhakikisha watu wanarejea nyumbani salama kila siku,” alisema Temba.
Aliongeza kuwa mwitikio mzuri wa washiriki na kuvuka lengo la mafunzo vinaonesha umuhimu wa kuendeleza programu hiyo kwa kushirikiana na wadau wengine.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Tanzania Red Cross Society, Lucia Pande, alisema usalama barabarani ni jukumu la kila mmoja na kwamba kuwapatia waendesha pikipiki stadi za huduma ya kwanza kunaongeza uwezo wa jamii kukabiliana na dharura.

Alisema waendesha pikipiki mara nyingi huwa miongoni mwa watu wa kwanza kufika katika maeneo ya ajali, hivyo maarifa ya huduma ya kwanza yanaweza kusaidia kutoa msaada wa haraka kwa waathirika kabla ya kufikishwa hospitalini.

Katika hatua nyingine, TBL imeendelea kuhamasisha matumizi sahihi ya barabara na maamuzi yenye uwajibikaji, ikisisitiza kuwa unywaji wa pombe na uendeshaji wa pikipiki haviendani.

Kampuni hiyo imesema itaendelea kushirikiana na wadau kupanua programu za elimu ya usalama barabarani na huduma ya kwanza ili kuongeza uelewa na kujenga jamii yenye uwezo zaidi wa kuzuia na kukabiliana na ajali.

Matokeo ya Wilaya;

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: