Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Benki ya Exim Tanzania imezindua kampeni ya miezi mitatu inayolenga kuhamasisha wateja kutumia huduma za kibenki za kidijitali, huku ikitoa fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo Sh milioni 15.

Kampeni hiyo inayojulikana kwa jina la *‘Maliza Kirahisi Kidigitali-Kamata Kitita’* itaanza Novemba 2026 hadi Februari 2027, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo kuimarisha matumizi ya teknolojia katika utoaji wa huduma za kifedha.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mifumo Mbadala ya Kidijitali wa Benki ya Exim Tanzania, Silas Matoi, alisema wateja watapata nafasi ya kujishindia zawadi kupitia droo za kila wiki, kila mwezi na droo kuu ya mwisho wa kampeni.

Alisema katika droo za kila wiki, wateja 30 watajishindia Sh 50,000 kila mmoja, huku washindi 10 wa droo za kila mwezi wakipata Sh 500,000 kila mmoja.

Aidha, katika droo kuu, washindi watatu watajishindia zawadi za Sh milioni tano, milioni 10 na milioni 15 kulingana na nafasi zao.

Matoi alisema kampeni hiyo inalenga kuwahamasisha wateja kufanya miamala yao ya kila siku kupitia njia za kidijitali, ambazo zinawawezesha kupata huduma kwa haraka na urahisi bila kulazimika kutembelea matawi ya benki.

Alitaja njia hizo kuwa ni pamoja na Exim Pay, huduma ya USSD kupitia namba *150*11#, Internet Banking, Exim WhatsApp Banking, Exim Wakala na Exim Mastercard.

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Kauthar D'souza, alisema kampeni hiyo inalenga kuongeza matumizi ya huduma za kidijitali kwa kuwapa wateja motisha ya kushiriki katika miamala yao ya kawaida na kupata nafasi ya kushinda zawadi.

Aliwahimiza wateja kutumia huduma hizo na kuzingatia vigezo na masharti ya kampeni ili kunufaika na fursa zilizopo.

Naye Afisa Mkaguzi wa Michezo ya Kubahatisha, Pendo Albert Mfuru, alisema droo za kampeni hiyo zitaendeshwa kwa mfumo wa kielektroniki unaochagua washindi kwa nasibu chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.

Alisema usimamizi huo unalenga kuhakikisha mchakato wa kupata washindi unafanyika kwa haki na uwazi, huku washiriki wanaotimiza vigezo na masharti wakipata nafasi sawa ya kuwania zawadi.

 Kampeni hiyo ni sehemu ya juhudi za Benki ya Exim Tanzania kuendelea kuwekeza katika mifumo ya kisasa na kupanua upatikanaji wa huduma za kifedha kupitia teknolojia.

Benki ya Exim Tanzania ilianzishwa mwaka 1997 na inatoa huduma kwa watu binafsi na biashara. Mbali na Tanzania, benki hiyo inaendesha shughuli zake Comoros, Djibouti na Uganda, pamoja na kuwa na ofisi ya uwakilishi nchini Ethiopia.

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: