Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa akiwasili ghala ya Serikali iliyopo Handeni akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya hiyo Ndugu Godwin Gondwe.
  Mheshimiwa Bashungwa akiikagua moja ya mashine zilizopo katika ghala.
 Wafanyakazi wa ghala wakimuonyesha mihogo iliyokwishapakiwa kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi.
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akimueleza Naibu waziri wa Kilimo namna mhogo unavyopokelewa na kuanza kuandaliwa.
 Mheshimiwa Bashungwa akishuhudia mkonge ukichakatwa alipozuru mashamba ya Kwaraguru.
 Mmoja ya watumishi akimuelezea Naibu Waziri shughuli za uchakataji mkonge inavyofanyika
Naibu Waziri akifanya kikao na uongozi wa Wilaya ya Handeni.

Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa amesisitiza umuhimu wa kila wilaya kuwa na kiwanda cha kuongeza thamani kwa mazao ya kimkakati. 

Bashungwa aliye mkoani Tanga katika ziara ya kikazi ya siku moja aliyasema hayo wakati alipotembelea ghala ya Serikali iliyopo Kwa Chaga, wilaya ya Handeni ambapo aliweza kushuhudia zao la muhogo likiandaliwa kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Ndugu Godwin Gondwe alieleza namna ambavyo wilaya yake imekuwa ikitafuta masoko kabla ya msimu wa kilimo kuanza hali inayowasaidia kufahamu zao gani lina uhitaji mkubwa sokoni hivyo kuwawezesha wakulima kuwa na uhakika wa kipato kizuri msimu wa mavuno. 

Wilaya ya Handeni imepata soko la mhogo nchini China na imekwishasafirisha tani 200 mpaka sasa huku ikitarajiwa kusafirisha nyingine Zaidi. Mheshimiwa Bashungwa aliupongeza uongozi wa Wilaya kwa kutumia mfumo huu na kusema kuna haja ya maeneo mengine nchini kujifunza toka Handeni

Katika ziara hiyo Naibu Waziri alitembelea pia kiwanda cha kuchakata mkonge kilichopo katika mashamba ya Kwaraguru ambako aliweza kujionea shughuli za kiwanda hicho na kuukumbusha uongozi azma ya Serikali ya awamu ya tano kuona uanzishwaji viwanda unaenda na kukua kwa shughuli za kilimo. Mheshimiwa Bashungwa anatarajiwa kuendelea na ziara ya mikoa ya Kaskazini kwa kwenda mkoa Kilimanjaro hapo kesho.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: