MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella  akizungumza wakati uzinduzi wa mradi wa afya kamilifu wa huduma na matibabu ya kufubaza virus vya Ukimwi katika mikoa ya Tanga na Zanzibar.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Mkurungenzi Mkazi wa Amref Health Afrika Dkt Florence Temu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi huo.
MENEJA wa mradi wa Afya kamilifu Dkt Edwin kilimba akizungumza wakati wa uzinduzi huo. 
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizundua mradi huo.
Sehemu ya wakuu wa wilaya waliohudhuria uzinduzi huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa, Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Lushoto January Lugangika.
=
Sehemu wa washiriki wakifuatilia uzinduzi huo.
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Amrefu kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kulia ni Mkurungenzi Mkazi wa Amref Afrika Dkt Florence Temu.
Picha ya pamoja.
SHIRIKA la Amref Health Afrika leo limezindua mradi wa Afya Kamilifu wa huduma na matibabu ya kufubaza Virusi vya Ukimwi katika mkoa wa Tanga na Visiwani Zanzibar utakaokuwa wa miaka mitano 

Akizungumza wakati akizundua mradi huo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella aliwataka viongozi wa mkoani humo wametakiwa kuhamasisha waumini wao kuona umuhimu wa kupima kwa hiari afya zao ikiwemo kuacha tabia ya kuwanyanyapaa waathirika wa UKIMWI walioko katika jamii.

Alisema kuwa viongozi hao wanajukumu kubwa la kuhakikisha wanawasaidi waumini wao kuona umuhimu wa kutambua afya zao na wale walioathirika wajitambue na kuwa tayari kuanza matibabu ya dawa.

“Licha ya mkoa wa Tanga kiwango cha maambukizi kufikia asilimia 5% inahitajika nguvu ya ziada katika kuhakikisha tunapunguza kasi ya maambukizi mpya kwa kuanza kufanyia utafiti maeneo ambayo ni visababishi vya ugonjwa huo”alisema Mkuu wa mkoa huyo.

Alisema kuwa kwani tafiti zinaonyesha kuwa nchini Tanzania kuna watu takribani mil 1,4 ambao wanaishi na VVU lakini wanaotumia dawa za kufubaza ugonjwa huo ni wachache sana hivyo lengo la serikali ni kuwatambua wao hao na kuhakikisha wanatumia dawa ili kupunguza kasi ya maambukizi mpya. 

Kwa upande wake Mkurungenzi Mkazi wa Amref Health Afrika Dkt Florence Temu
alisema kuwa mradi wa afya kamilifu unalenga katika kuongeza idadi ya watu wanaojijua kuwa wanaishi na VVU na UKIMWI wanaopata huduma za matibabu ya kufubaza virus hivyo ili kuhakikisha vinafubazwa.

Alisema kuwa wamelenga katika kuhakikisha kwamba katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa mradi huo watu wote wanaoishi na VVU na UKIMWI wanaishi mkoani Tanga kujua hali zao na kupata matibabu kamilifu.

“Katika kipindi cha miezi sita ya utekelezaji wa mradi huo tumeweza kubaini kesi za waathirika wa UKIMWI zaidi 3000 ,na wameweza kuanzishiwa matibabu ya dawa za kufubaza ugonjwa huo mara baada ya kubaini kuwa wameathirika”alisema Dkt Temu.

Hata hivyo Meneja wa mradi wa Afya kamilifu Dkt Edwin kilimba alisema kuwa mradi huo utaimarisha ufuatiliaji na tathimini kiasi cha kupata taarifa halisi za maendeleo katika muda halisi ili kuimarisha usimamizi bora

“Mradi unaunga mkono malengo mapya ya progamu ya pamoja ya Umoja wa Mataifa kuhusu VVU/UKIMWI kwa kupanua tiba ya kufubaza virusi ili kumaliza janga la ugonjwa huo hapa nchini ifikapo mwaka 2030”alisema Dkt Kilimba.

Vile vile alisema kuwa mradi huo utaweza kuimarisha mifumo ya afya kwa watu wanaoishi na UKIMWI kwa ajili ya kuwapatia huduma za matunzo na tiba katika vituo vya afya ili kuweza kufanyakazi kwa ufanisi hasa katika wilaya ambazo mradi huo unafika.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: