Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini, TMA, Dkt. pascal Waniha akizungumza na waandishi wa Habari juu ya uwepo wa Kimbunga Kenneth, kinachotarajiwa kutokea April 26,2019 na Athari zake na kueleza jinsi ambavyo wananchi wanavyotakiwa kuchukua tahadhari ikiwa ni moja ya njia ya kuondoa changamoto zinazoweza kujitokeza.
---
Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania TMA imewataka wananchi kuchukua tahadhari na kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa na ushauri unaotolewa na mamlaka hiyo ili kupunguza athari zinazowezeza kujitokeza endapo kutakuwa na uwepo wa kimbunga Kenneth.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo Aprili 24, 2019 Kaimu Mkurugenzi mkuu wa TMA Tanzania Dkt. Pascal Waniha amesema wanatoa ufafanuzi huo ikiwa ni moja ya njia ya kuondoa changamoto zinazoweza kujitokeza.

Kwa Mujibu wa Dkt Pascal Waniha kimbunga Kenneth kinatarajiwa kuambatana na upepo mkali wa kasi ya kilometa 80 kwa saa ambacho kitaathiri zaidi katika maeno ya Mtwara, Lindi Pwani na maeneo jirani ya mikoa hiyo kwa umbali wa kilometa 500.

Amesema, Kimbunga Kenneth kilichopo eneo la kaskazini magharibi mwa kisiwa cha Madagascar kinaambatana na mvua kubwa na upepo mkali huku eneo la pwani ya Kusini yaani Lindi na Mtwara kinatarajiwa kufikiwa na hali hiyo.

"Kimbunga hicho kinaendelea kutawala mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa hapa nchini, hivyo kisababisha ongezeko la mvua zinazoambatana na ngurumo za radi pamoja na upepo mkali kadri kinavyokaribia maeneo ya ukanda wa pwani", amesema Dk Waniha.

Ameongeza, kama kimbunga cha Kenneth kitaingia nchi kavu kwa nguvu inayotarajiwa baei madhara makubwa kwa maisha ya watu na Mali yanaweza kutokea ikiwa ni pamoja na mtawanyiko mkubwa wa mafuriko, uharibifu wa miundombinu, kuongezeka kwa kina cha Maji baharini katika kipindi kifupi, kuathirika kwa shughuli za usafirishaji kwa njia ya anga, Maji na hata nchi kavu.

Pamoja na mambo mengine Dkt. Waniha amebainisha athari ambazo zinaweza kujitokeza ikiwemo mafuriko na uharibifu wa mali na makazi .

Katika hatua nyingine Dkt Waniha amebainisha sababu za vimbunga vinavyotokea maeneo mbalimbali ya dunia kupewa majina hususan ya binadamu ambapo amesema kuwa majina vinapewa kutokana na wadau wanaokutana kujadili masuala hayo ya vipunga ambap Tanzania ni moja ya nchi ambazo zinashiriki katika kujadili masuala hayo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: