Kila tarehe 8 Agosti, Tanzania huadhimisha Nane Nane kwa kutambua mchango wa wakulima katika kulisha taifa, kuimarisha maisha ya wananchi na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Kilimo ni moja ya sekta muhimu kwa uchumi wa Tanzania, kikichangia takribani 26% ya Pato la Taifa (GDP) na kuajiri zaidi ya 61% ya Watanzania. Pia kinatoa malighafi muhimu kwa viwanda vya chakula na vinywaji, nguo na bidhaa za mauzo ya nje.
Hata hivyo, mustakabali wa kilimo hautegemei uzalishaji pekee. Unahitaji ushirikiano kati ya wakulima, Serikali, taasisi za utafiti, taasisi za kifedha, washirika wa maendeleo na sekta binafsi ili kuongeza uzalishaji, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuhakikisha upatikanaji wa masoko.

Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL PLC) inaendelea kushirikiana na wakulima kupitia Mpango wa Smart Agriculture. Mwaka 2025, TBL ilishirikiana na zaidi ya wakulima wadogo 2,500 kwa kuwapatia ushauri wa kitaalamu, mafunzo ya kiufundi na programu za kuwawezesha kiuchumi.
Ushirikiano huu unalenga kuwasaidia wakulima kuongeza uzalishaji, kuboresha ubora wa mazao na kutumia mbinu endelevu za kilimo, huku ukiimarisha upatikanaji wa malighafi zinazozalishwa nchini.

Dhamira hii imeendelea kuimarishwa kupitia Kiwanda cha Kilimanjaro Malting, ambacho kilikamilisha mwaka wake wa kwanza wa uzalishaji mwaka 2025. Kiwanda hicho kinaongeza matumizi ya shayiri inayolimwa nchini na kinatarajiwa kuongeza ununuzi wa shayiri ya ndani pamoja na kupanua fursa za kilimo cha mkataba kwa wakulima wa Tanzania.
Kwa TBL, mafanikio ya wakulima ni sehemu ya kujenga mnyororo imara wa thamani. Wakulima wanapopata maarifa, teknolojia, masoko na fursa za kifedha, wanaweza kuongeza uzalishaji na kujenga biashara za kilimo zenye uwezo wa kukabiliana na changamoto.

Nane Nane ni wakati wa kutambua mafanikio ya wakulima, lakini pia kutazama ushirikiano unaohitajika kuujenga mustakabali wa kilimo Tanzania.Mustakabali wa kilimo nchini unategemea ushirikiano. Kwa kuwaunganisha wakulima, sekta ya viwanda, Serikali, taasisi za utafiti na washirika wa maendeleo, Tanzania inaweza kuongeza uzalishaji, kuimarisha ustahimilivu na kujenga thamani zaidi katika uchumi wa kilimo.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: