Benki ya Exim Tanzania imehitimisha mafunzo kwa wanawake wajasiriamali 50 waliofanikiwa kukamilisha programu ya wiki sita ya Women Empowerment Programme (WEP) 2026 jijini Dar es Salaam.Utekelezaji wa programu hii kupitia mpango wao wa kurudisha kwa jamii wa Exim Cares unalenga kuwajengea wanawake wajasiriamali maarifa na ujuzi kwa vitendo na kuimarisha biashara zao, ikiwemo usimamizi wa fedha, uandaaji wa bajeti, kuwafahamu wateja wao, kutambua fursa za soko na kupanga mikakati ya ukuaji endelevu wa biashara.
Programu hii haiishii kwenye mafunzo pekee. Wahitimu wanaunganishwa na fursa, mitandao ya masoko pamoja na huduma za kifedha zinazoweza kuwasaidia kuchukua hatua inayofuata katika safari zao za biashara.
Wakati wakiwapongeza wanawake hao 50, Benki ya Exim inaendelea kutarajia kuona biashara zao zikikua, zikitoa fursa kwa wengine na kuleta matokeo chanya katika familia na jamii zinazowazunguka.






Toa Maoni Yako:
0 comments: