
Ndugu Deo Masuki anatangaza kwa masikitiko makubwa kifo cha kaka yake mpendwa, Elihuruma Sifael Masuki, kilichotokea tarehe 22 Oktoba 2026 jijini Dar es Salaam.
Msiba upo nyumbani kwa marehemu, Kimara Temboni (St. Augustine), Dar es Salaam. Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa tarehe 30 Oktoba 2026 kuelekea mkoani Kilimanjaro, ambapo mazishi yatafanyika Jumamosi, tarehe 31 Oktoba 2026, katika eneo la Kilema Pofu, Himo, mkoani Kilimanjaro.
Tangazo hili liwafikie Ndugu, Jamaa na Marafiki.
“BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na lihimidiwe.” (Ayubu 1:21).


Toa Maoni Yako:
0 comments: