Articles by "MAMA SAMIA SULUHU"
Showing posts with label MAMA SAMIA SULUHU. Show all posts
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na Dkt. Khalid Bin Mohammed Al Attiyah, Mwenyekiti wa Kampuni ya Thirty Five Investment Holding inayoshughulika na masuala ya Kilimo, Uvuvi Bahari Kuu, Ufugaji, Madini na Miundombinu kutoka Qatar, Ikulu, Jijini Dar es Salaam, tarehe 06 Novemba, 2026.
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa kwenye picha na Dkt. Khalid Bin Mohammed Al Attiyah, Mwenyekiti wa Kampuni ya Thirty Five Investment Holding ya Qatar mara baada ya mazungumzo yao, Ikulu, Jijini Dar es Salaam, tarehe 06 Novemba, 2026.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa kampuni ya Thirty-Five Investment Holding kutoka Qatar, Dkt. Khalid bin Mohammed bin Abdullah Al Attiyah, kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji nchini.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Novemba 6, 2026, Dkt. Al Attiyah ameeleza nia ya kampuni yake kuwekeza katika sekta za kilimo na ufugaji, ikiwemo uzalishaji wa sukari na ufugaji wa ng'ombe katika eneo la Kongwa mkoani Dodoma.

Katika sekta ya uvuvi, mazungumzo yamejikita katika fursa za uvuvi wa bahari kuu pamoja na uwekezaji katika mitambo ya uchakataji na miundombinu ya kuhifadhi samaki katika Bandari ya Uvuvi Kilwa.

Aidha, mwekezaji huyo ameeleza kuwa kampuni yake inatathmini fursa za kuwekeza katika miundombinu ya usafiri Zanzibar, ambako majadiliano kati ya timu yake na wataalamu wa taasisi husika kuhusu miradi inayopendekezwa yameanza.

Kwa upande wake, Rais Samia amezitaka taasisi zinazohusika kuendeleza majadiliano na kampuni hiyo kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni zilizopo ili kubaini fursa za uwekezaji zinazoweza kutekelezwa kwa manufaa ya pande zote.
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa kwenye mazungumzo na Mhe. Noluthando Mayende-Malepe, Balozi wa Afrika Kusini anayemaliza muda wake nchini Tanzania, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 06 Novemba, 2026.

Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa kwenye picha na Mhe. Noluthando Mayende-Malepe, Balozi wa Afrika Kusini anayemaliza muda wake nchini Tanzania, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 06 Novemba, 2026.
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiagana na Mhe. Noluthando Mayende-Malepe, Balozi wa Afrika Kusini anayemaliza muda wake nchini Tanzania, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 06 Novemba, 2026.

Na Mwandishi Wetu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Noluthando Mayende-Malepe, anayemaliza muda wake wa utumishi nchini.

Katika mazungumzo yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Novemba 6, 2026, Balozi Mayende-Malepe amemshukuru Rais Samia, Serikali na wananchi wa Tanzania kwa ushirikiano na ukarimu alioupata katika kipindi cha miaka minne ya utumishi wake nchini.

Balozi huyo amesema Tanzania imekuwa na nafasi ya kipekee katika maisha na utumishi wake wa kidiplomasia kutokana na ukarimu wa Watanzania pamoja na uhusiano wa kihistoria na kindugu uliopo kati ya Tanzania na Afrika Kusini, ulioasisiwa wakati wa harakati za ukombozi wa Bara la Afrika.

Amesema anaondoka nchini akiwa na kumbukumbu nzuri, huku akiipongeza Tanzania kwa mchango wake katika masuala ya kikanda na kimataifa. Aidha, amezikaribisha kampuni za Tanzania kutumia fursa zilizopo kuwekeza na kufanya biashara nchini Afrika Kusini.

Kwa upande wake, Rais Samia amempongeza Balozi Mayende-Malepe kwa kuhitimisha utumishi wake na kumshukuru kwa mchango wake katika kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili.

Amesema biashara kati ya Tanzania na Afrika Kusini imeendelea kuongezeka katika kipindi cha utumishi wa Balozi huyo, akisisitiza umuhimu wa kutumia fursa zilizopo kukuza zaidi biashara na uwekezaji kwa manufaa ya mataifa yote mawili.

Balozi Mayende-Malepe aliwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais Samia Agosti 25, 2022 na kuhudumu nchini kwa miaka minne.

Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipiga kura kwenye Kituo cha kupigia kura cha Ofisi ya Kijiji cha Chamwino mkoani Dodoma, tarehe 04 Novemba, 2026 katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Chamwino. Uchaguzi huo unafanyika kufuatia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Mhe. Deogratius Ndejembi kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
By Our Correspondent, Dar es Salaam.

Tanzania and Angola have agreed to strengthen diplomatic relations and expand economic cooperation in trade, investment, transport, energy, mining and health, as part of efforts to deepen bilateral ties between the two countries.

Among the key steps agreed upon is Tanzania’s decision to reopen its embassy in Luanda, Angola, to strengthen diplomatic engagement and facilitate cooperation in various strategic sectors.

The announcement was made by President Samia Suluhu Hassan during a joint press conference with her Angolan counterpart, President João Manuel Gonçalves Lourenço, who is in Tanzania for a State Visit, at State House in Dar es Salaam.

President Lourenço’s visit is the first by an Angolan President since the country’s founding leader, the late Dr António Agostinho Neto, visited Tanzania in 1979.

President Samia said trade between the two countries remained low despite their longstanding relations and the numerous economic opportunities available in both markets.

She said Tanzania had invited Angola to source agricultural products from its market, while Tanzania would explore opportunities to import petroleum products and fertilisers from Angola.

The two countries also agreed to pursue plans to connect Angola’s Benguela Railway with the Tanzania-Zambia Railway Authority (TAZARA) through Zambia and the Democratic Republic of Congo.

The proposed railway connection is expected to facilitate freight transportation between the Atlantic port of Lobito in Angola and the Indian Ocean port of Dar es Salaam.

On air transport, President Samia said the two countries intended to establish direct flights between Dar es Salaam and Luanda to facilitate travel, trade and people-to-people exchanges without requiring passengers to transit through third countries.

“We now want to establish direct flights between Dar es Salaam and Luanda,” she said.

In the energy sector, President Samia revealed that the Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) had started assessing investment opportunities in Angola’s Lobito Refinery.

The two countries also agreed to exchange expertise in mineral value addition and strengthen the technical capacity of specialists and small-scale miners to enable them to benefit more from their mineral resources.

For his part, President Lourenço acknowledged Tanzania’s historical contribution, under its founding President, the late Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, to Angola’s liberation struggle led by the late Dr António Agostinho Neto.

He said the current leadership of both countries had a responsibility to build on the historic friendship by promoting economic growth and improving the living standards of their people.

On health cooperation, President Lourenço said Angola was interested in recruiting Tanzanian health professionals on contractual terms to address personnel shortages in its expanding hospital network.

He added that the two countries would also cooperate through the exchange of expertise and training at medical education institutions, alongside efforts to improve maternal and child healthcare services.

“However rich our countries may be in resources, we cannot develop our economies and improve our people’s lives on our own,” President Lourenço said, emphasising the importance of African countries combining their capabilities to address development challenges.

During the visit, the two leaders also witnessed the signing of agreements and memoranda of understanding covering cooperation in aviation, communications and meteorology.

President Lourenço is expected to travel to Dodoma tomorrow, where he will join President Samia for the inauguration of the Government City in Mtumba.
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na mgeni wake Mhe. João Manuel Conçalves Lourenço, Rais wa Jamhuri ya Angola wakiwa katika Stesheni ya Magufuli tayari kwa safari ya kuelekea Jijini Dodoma kwa ajili ya uzinduzi wa Mji wa Serikali Mtumba,tarehe 30 Oktoba, 2026.
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa na mgeni wake Mhe. João Manuel Lourenço, Rais wa Jamhuri ya Angola, wakisafiri kwa treni ya mwendo kasi (SGR) kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kwenye Uzinduzi wa Mji wa Serikali Mtumba, leo tarehe 30 Oktoba, 2026.
Na Mwandishi Wetu, Morogoro.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Queen Cuthbert Sendiga, na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Mongoso Wambura, kufuatia vifo vya watu 32, wakiwemo askari polisi watatu, vilivyotokana na ajali mbili tofauti za barabarani mkoani humo.

Ajali hizo zimetokea usiku wa kuamkia Oktoba 9, 2026, na kusababisha vifo hivyo pamoja na majeruhi ambao Rais amewatakia uponyaji wa haraka.

Katika salamu zake za rambirambi, Rais Dkt. Samia ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu, akiwataka kuwa na nguvu, subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Aidha, amewaombea faraja wafiwa wote na kuwatakia majeruhi kupona haraka ili waweze kurejea katika shughuli zao za kila siku.

Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Samia amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea kusimamia na kutekeleza sheria za usalama barabarani kwa lengo la kupunguza ajali na kulinda maisha ya wananchi.

Vilevile, amewasihi madereva na watumiaji wengine wa barabara kuzingatia sheria, kuchukua tahadhari na kuwajibika wanapokuwa barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika.

Rais Dkt. Samia amesisitiza umuhimu wa kila mtumiaji wa barabara kutambua wajibu wake katika kulinda maisha na usalama wa wengine.

Amehitimisha salamu zake kwa kumwomba Mwenyezi Mungu azipumzishe roho za marehemu mahali pema peponi. Amina.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mama Fatma Karume, mjane wa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika salamu zake za rambirambi, Rais Samia ametoa pole kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Amani Abeid Karume, pamoja na familia, ndugu, jamaa na wananchi wote wa Zanzibar kutokana na msiba huo.

Aidha, Rais Samia amewaombea wafiwa wote subira na faraja katika kipindi hiki cha majonzi, huku akimuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi.

“Inna lillahi waina ilayhi raajiun.”

President of the United Republic of Tanzania, Dr Samia Suluhu Hassan, has expressed her sincere gratitude to Tanzanians and people around the world for the messages of condolence, prayers, love and support following the death of her beloved husband, Mr Hafidh Ameir Hassan.

Mr Hafidh passed away in Zanzibar on September 7, 2026.

In a message of appreciation, President Samia said she and her family have been deeply touched by the kindness and compassion shown to them during this difficult period.

She extended her appreciation to Heads of State and Government, national leaders, members of the diplomatic community, religious leaders and all Tanzanians for standing with her family and providing strength and comfort as they conclude three days of mourning.
Mheshimiwa Felix Antoine Tshisekedi Tshilombo, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) akimfariji Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kuwasili nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 08 Septemba, 2026 kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, tarehe 07 Sept, 2026.

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Afrika CDC) Dkt. Jean Kaseya akimfariji Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuwasili nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 08 Septemba, 2026, kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan, aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, tarehe 07 Sept, 2026.

Mtume Boniface Mwamposa pamoja na Mchungaji Tony Kapola wakimfariji Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuwasili nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 08 Septemba, 2026, kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan, aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, tarehe 07 Sept, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Burundi, Mhe. Evariste Ndayishimiye, akimfariji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 08 Septemba 2026, kufuatia kifo cha mume wake, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba pamona na Viongozi mbali mbali wa Vyama na Serikali na Wananchi, wakimfariji Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walipofika nyumbani kwake Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja, kufuatia kufiwa na Mume wake Maalim Hafidh Ameir Hassan aliyefariki Dunia katika Hospitali ya Mzena Zanzibar, tarehe 07 Sept, 2026.























Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshuhudia uapisho wa Mheshimiwa Deogratius John Ndejembi kuwa Makamu wa Rais, na kumuasa kutekeleza dhamana hiyo kwa uzalendo, bidii, uadilifu na uwajibikaji.

Akizungumza katika hafla ya uapisho leo, tarehe 29 Agosti, 2026, Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma, Rais Dkt. Samia amesema nafasi ya Makamu wa Rais inahitaji uongozi wenye kuunganisha watu, kusimamia utekelezaji wa shughuli za Serikali na kutanguliza maslahi ya Taifa.

“Cheo si ufalme, ni dhamana. Dhamana uliyopewa ni ya kuwatumikia Watanzania,” amesema Rais Dkt. Samia.

Rais Dkt. Samia amesema uzoefu wa Mheshimiwa Ndejembi katika nafasi mbalimbali alizowahi kushika Serikalini, pamoja na bidii, uwezo wa kujifunza, kufuatilia na kusimamia vyema dhamana anazopewa, unampa msingi mzuri wa kutekeleza wajibu wake mpya katika nafasi ya Makamu wa Rais.

Aidha, amemtaka Makamu wa Rais kuendelea kuimarisha umoja, mshikamano, ushirikiano na utulivu, huku akishirikiana na viongozi wengine katika kutekeleza majukumu ya Serikali.

Ameongeza kuwa, matarajio ya wananchi kuhusu maendeleo yanaweza kufikiwa kwa Serikali na viongozi wake kufanya kazi kwa ushirikiano, nidhamu na uongozi bora katika kila ngazi.

Rais Dkt. Samia amesema utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unahitaji uongozi unaosukuma matokeo na kutanguliza maslahi ya wananchi.

Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Samia ameipongeza Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi kwa kuridhia jina la Mheshimiwa Ndejembi, akisema uteuzi wake umezingatia uwezo, uzoefu na sifa za kiuongozi.

Amesema umri wa Mheshimiwa Ndejembi unampa nafasi ya kutumia nguvu na maarifa yake katika kulitumikia Taifa, huku akimtaka kuendelea kujifunza na kukua katika majukumu yake mapya. Mheshimiwa Ndejembi ameapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi, na baadaye uteuzi wake kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Na Janeth Raphael - MichuziTv -Ikulu Chamwino

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema uamuzi wa kumteua Deogratius Ndejembi kuwa Makamu wa Rais ulizingatia sifa, uzoefu na uwezo wake wa kubeba dhamana kubwa ya uongozi wa taifa.

Rais Samia amesema nafasi hiyo imekabidhiwa tena kwa kijana, akimtaka Ndejembi kutumia fursa hiyo kujifunza, kukua kiakili na kutekeleza majukumu yake kwa weledi, utii na uaminifu kwa maslahi ya Watanzania.

Akizungumza leo, Agosti 29, 2026, katika hafla ya kumuapisha Ndejembi kuwa Makamu wa Rais iliyofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma, Rais Samia amesema uamuzi wa kumrudisha kijana katika nafasi hiyo ulifanyika kwa kauli moja.

“Kwa kauli moja tuliamua kuirudisha nafasi ya Makamu wa Rais kwa vijana na tuendelee kulea. Imetoka kwa kijana na tumeirudisha kwa kijana. Tunakuomba kijana (Ndejembi) ukakue sio kwa umri bali ukakue kiakili, tumekupa majukumu makubwa ni imani yangu utaweza,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema Ndejembi alipata uungwaji mkono wa wabunge kwa kauli moja kutokana na sifa alizonazo zinazomfanya astahili kushika nafasi hiyo.

“Wabunge walimpitisha Deogratius Ndejembi kwa kauli moja kwa kuzingatia sifa za Makamu wetu wa Rais,” amesema.

Amesema kabla ya kufikia nafasi ya Makamu wa Rais, Ndejembi amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi serikalini na katika sekta binafsi, akieleza kuwa uzoefu huo utakuwa nyenzo muhimu katika utekelezaji wa majukumu yake mapya.

“Makamu wa Rais Deogratius Ndejembi, kabla ya wadhifa huu, ulishika nafasi mbalimbali za uongozi serikalini na sekta binafsi. Sina shaka kwamba uzoefu huo utakusaidia kutekeleza majukumu ya dhamana hii uliyopewa,” amesema Rais Samia.

Kwa mujibu wa Rais Samia, hakuna shule maalumu inayomwandaa mtu kuwa Makamu wa Rais, bali uwezo wa kutekeleza majukumu hayo unajengwa kupitia sifa binafsi, bidii, weledi, nidhamu pamoja na utayari wa kujifunza na kusimamia utekelezaji wa majukumu.

Amesema sifa hizo zitamsaidia Ndejembi kutekeleza ipasavyo dhamana aliyopewa na taifa.

Rais Samia pia amesema uzoefu wa Ndejembi ndio uliowafanya viongozi kutokuwa na kusita katika kupitisha jina lake wakati wa kutafuta mtu wa kujaza nafasi hiyo.

“Kwa uzoefu huo ndio maana wakati tunatafuta mtu wa kujaza nafasi hii, hatukusita hata kidogo kupitisha jina lako. Hivyo ni matamanio na matarajio yetu sote Watanzania utalitumikia vyema, kwa utii, uaminifu, utu, busara, uzalendo, hekima, maarifa na uzoefu ulio nao, ukimtanguliza Mungu mbele na kwa maslahi ya taifa,” amesema.

Katika hatua nyingine, Rais Samia amemtaka Ndejembi kwenda kuwatumikia Watanzania wote bila kujali tofauti zao, akisisitiza umuhimu wa kiongozi kuweka mbele maslahi ya taifa.

“Nenda ukawatumikie Watanzania bila kujali tofauti zao,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema serikali ina kazi kubwa ya kutekeleza ahadi zilizowekwa kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2025–2030, sambamba na kuanza utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya miaka 25 ijayo.

Amesema dira hiyo imebeba matarajio makubwa ya maendeleo kwa wananchi, hivyo utekelezaji wake unahitaji umoja, mshikamano, ushirikiano, utulivu na uongozi bora.

“Ili tuweze kutekeleza haya yote kwa maslahi ya wananchi wetu na taifa kwa ujumla, tunahitaji umoja, mshikamano, ushirikiano, utulivu na uongozi bora,” amesema.

Uapisho wa Ndejembi unafungua rasmi ukurasa mpya katika safari yake ya uongozi wa kitaifa, huku akianza kutekeleza majukumu ya Makamu wa Rais chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan